Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae ameomba wafanyibiashara wote wa jamii ya Kisii ambao wamewekeza biashara zao katika sehemu mbalimbali nchini kuhudhuria mkutano mkubwa wa kibiashara katika chuo kikuu cha Kisii kuanzia tarehe 25 hadi 27 Februari.
Kulingana na Ongwae, ni vizuri wafanyibiashara hao kuhudhuria mkutano huo ili kutoa himizo kwa wafanyibiashara wengine kuekeza zaidi kwa biashara na kueleza umuhuimu wa kufanya biashara.
Akihutubia waandishi wa habari siku ya Jumapili mjini Kisii, Ongwae aliomba kila mwanabiashara ambaye amewekeza katika sehemu mbalimba nchini kujaribu kila awezalo kuhakikisha kuhuduria mkutano huo.
Ongwae alisema tayari wameongea na Rais Uhuru Kenyatta ili kuhudhuria mkutano huo, huku akisema Rais alikubali kuhudhuria mkutano huo.
“Wale wote ni wawekezaji wa biashara ambao hutoka katika jamii yetu ya Kisii, naomba mhudhurie mkutano mkubwa wa kibiashara ambao utaandaliwa katika chuo kikuu cha Kisii mwezi huu,” alisema Ongwae.
Ongwae, aliomba kila mkazi kujiunnga na serikali yake ili kufanya maendeleo pamoja na kuhakikisha kaunti hiyo imesonga mbele katika maendeleo kwani serikali yake iko tayari kuimarisha biashara.