Wafanyibiashara watano wanaotuhumiwa kughushi stakabadhi za upakuaji mizingo wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja kila mmoja.
Upande wa mashtaka uliambia mahakama siku ya Alhamisi kuwa washtakiwa Inukollu Venkata Sivakumar, Omprakash Lokpal Singh, Priscillan Okello, James Makokha na Antony Karugu wanadaiwa kughushi stakabadhi ya upakuaji mizigo mnamo Mei 15, 2015, katika kampuni ya Pacific International Line, hali iliyotajwa kama kukwepa kulipa ushuru.
Watano hao walikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu mkuu Susan Shitub.
Kesi hiyo itasikizwa Aprili 6, 2016.