Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Zaidi ya wafanyikazi 300 katika ujenzi wa barabara ya Dongo Kundu katika eneo la Miritini wamegoma kufuatia kucheleweshwa kwa malipo yao.

Wafanyakazi hao pia wanadai wanalipewa kiwango cha chini ikilinganishwa na wenzao wa maeneo mengine.

Vile vile wamelalamikia usalama wao wakati wakazi huku wakisistiza kuwa hakuna watu walio na ujuzi wa huduma ya kwanza na pia hawana mkataba wa kufanya kazi.

Haya ni kwa mujibu wa msemaji wa wafanyikazi hao Mwinyi Mohamed ambaye aliongeza kuwa hawatotishika na vitisho vya kufutwa kazi.

Naibu afisa wa wafanyikazi Janet Charo alisema siku ya Jumatano kuwa hana taarifa kuhusu tishio la wafanyikazi hao kufutwa kazi wala taarifa kuhusu malalamishi ya wafanyikazi hao na kusema kuwa usimamizi bado unashughulikia mshahara wao.