Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Vita dhidi ya ugonjwa wa saratani nchini Kenya vinazidi kukumbwa na changamoto tele baada ya mashine inayotumika kupunguza makali ya ugonjwa huo almaarufu radiotherapy katika hospitali kuu ya Kenyatta kufeli kwa mara ya tatu sasa.

Kulingana na daktari mkuu wa ugonjwa wa saratani katika hospitali ya Kenyatta Dkt Eliud Njuguna, moja ya mashine mbili za radiotherapy katika hospitali ya Kenyatta ilifeli siku ya Jumanne na kuwaathiri takriban wagonjwa 50 waliokuwa wakipokea matibabu.

"Tuna matumaini kwamba mashine itakuwa sawa ifikiapo siku ya Ijumaa. Changamoto kubwa itakuwepo iwapo wahandisi wanaoishugulikia watashindwa kuitengeza kwani itabidi tuite mtaalamu wa kutengeneza mashine hiyo kutoka nchini Tunisia, suala ambalo litachukua muda mrefu," alisema Dkt Eliud Njuguna.

Hata hivyo Njuguna alisema kuwa wamelazimika kutumia mashine mpya ya ugonjwa wa saratani iliyoletwa katika hospitali hiyo ya Kenyatta.