Wakaazi wa kaunti ya Mombasa wanaotumia kivuko cha feri cha Likoni wametahadharishwa dhidi ya mbinu mpya ambayo wahalifu wanatumia kuibia wakaazi hao wanapotumia kivuko hicho.
Kwa mujibu wa Afisa mkuu wa polisi katika stesheni ya Likoni Willy Simba.
Wahalifu hao wamebuni dawa maalum ya kupulizia watu na hususana huzitumia wakati wa usiku ambapo ukipuliziwa unadhoofika na hatimaye kulala na kuwapa nafasi ya kukupora.
Simba amesema kuwa visa hivyo vimeripotiwa mara kwa mara na kwa sasa maafisa wa usalama wanafanya uchunguzi wa kina kuhusu wahusika na kuhakikishia wakaazi kuwa watawakamata hivi karibuni.
Kwa sasa amewatahadharisha kuwa si vyema kutumia kivuko hichio wakati wa usiku ukiwa mtu mmoja na kusema kuwa iwapo utahitaji kutumia kivuko hicho wakati wa usiku basi ni bora umtafute rafiki wa karibu au jamaa yako mvuke naye.