Wahudumu wa kampuni za kuuza mafuta ya Petroli na Diseli mjini Mombasa, sasa wanalalamikia kupata hasara baada ya bei ya mafuta kushuka kote nchini.
Kulingana na Afisa msimamizi wa kampuni ya mafuta ya Gapco Oil iliyoko katika barabara ya Moi Avenue mjini Mombasa Vincent Ramu, kushuka kwa bei ya mafuta kumechangia magari mengi hasa ya uchukuzi wa umma kununua mafuta ya magari yao kwa watu binafsi na kuelekea biashara kushuka.
Katika mahojiano ya kipekee na mwanahabari wetu, Vincent amesema kuwa magari mengi wanayopokea katika vituo vyao ni yale ya kibinafsi pekee hali iliyopeleka biashara kushuka.
"Tangu bei ya mafuta ishuke kumepata hasara kubwa sana kwa sababu wateja tuopokea kwa sasa ni wale wa magari ya kibinafsi pekee wale wa magari ya umma wameelekea wa watu binafsi wao na vibali vya kufanya biashara hii, lakini bado tuko na matumaini kuwa biashara itaimarika," alisema Vincent.
Amesema kuwa sasa hawana budi ila kusubiri hadi tarahe 14 mwezi wa Februari iwapo sekta ya Kawi nchini itatangaza kupanda kwa bei ya mafuta ili kuwa afueni kwao.
Kwa sasa bei ya mafuta ya petroli ni shilingi 84.30 huku bei ya mafuta ya diseli ikiwa shilingi 72. 40 kwa kila lita.