Share news tips with us here at Hivisasa

Wahudumu wa matatu mjini Kisii wameomba serikali kuwajengea mzunguko wa barabara katika eneo la Hospitali ya Lamu mjini Kisii.

Wahudumu hao walisema kuwa hatua hiyo itasaidia katika kupunguza visa vya ajali vinavyoshuhudiwa katika eneo hilo mara kwa mara.

Kulingana na wahudumu hao, magari mengi hugongana kila wakati katika eneo hilo na kusababisha misongamano mikubwa.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu mjini Kisii, wahudumu hao, wakiongozwa na Godffrey Nyangeri, waliomba serikali kuwapunguzia visa vya ajali na misongamano ya magari kwa kuwajengea mzunguko katika eneo hilo.

“Eneo la Lamu ni eneo ambalo ni hatari kwetu sisi wahudumu wa matatu. Mara nyingi siku huwa haikamiliki bila magari kugongana katika eneo hili,” alisema Nyangeri, dereva.

Aliongeza, “Tunaomba serikali itujengee mzunguko ili kupunguza visa hivyo vya magari kugongana kila wakati.”