Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa Matopeni eneo la Kongowea, wanaishi kwa hofu ya kufurushwa kutoka kwa makaazi yao.

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatano,wakaazi hao walisema kuwa wameishi katika eneo hilo kwa muda mrefu, ila sasa wanatatizwa na taarifa zilizozagaa kuwa sehemu wanayoishi ni ya mmiliki wa kibinafsi, ambaye anataka kuchukua ardhi hiyo.

Wakiongozwa na Julius Kanampiu, mzee wa mtaa katika eneo hilo, wakaazi hao walimtaka Mbunge wa Nyali Hezron Awiti, kuwatetea bungeni ili wasinyanganywe ardhi hiyo.

“Tunamwomba mbunge wetu atuwasilishe kwa kututetea ili tusitimuliwe kutoka kwa ardhi hii,” alisema Awiti.

Kwa upande wake, mbunge huyo aliwaelezea wakaazi hao kuwa atahakikisha ardhi hiyo inasalia kuwa yao.