Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakaazi wa Molo wanamtaka kamishna wa kaunti ya Nakuru Joshua Nkanatha kuingilia kati swalala ukosefu wa usalama.

Wakiongea mjini Molo baada ya mkaazi mmoja kushambulia vijana na kukatwakatwa na majambazi, wakaazi hao walisema visa vya wizi vimekithiri sana eneo hilo.

“Watu kapsita saa hii huwezi chelewa nje, kichwa itaenda,” Joshua Makori alisema.

Wakaazi hao walisema kuwa polisi mjini humo hawana uwezo wa kufanya doria kila mahali na kwa hivyo kamishna anafaa kuingilia kati ili maafisa zaidi wa polisi watumwe kwenye maeneo ya mashinani.

“Mmoja wetu alitoweka mjini Elburgon, haijulikana alitekwa nyara na nani. Kamishna wa Nakuru lazima aje hapa ili tupate suluhu,” mkaazi mwingine alisema.

Juhudi za kuwasiliana na kamishna Nkanatha hazikufaulu.