Kufuatia kusimamishwa kazi kwa zaidi ya maafisa 8 wakuu wa shirika la bandari nchini, sasa baadhi ya wakazi kutoka kaunti ya Mombasa wamemtaka Rais kwa ushirikiano na wizara husika ya uchukuzi kumteua mwanamke kuchukua nafasi ya mkurugunzi mkuu katika shirika hilo.
Wakiongea siku ya leo katika eneo la Likoni wakazi hao wamesema kuwa ni wakati sasa kwa mwana mke kupewa nafasi ili kufanya juhudi za kupunguza visa vya ufisadi ambavyo vinadaiwa kukita mizizi katika shirika hilo kubwa zaidi nchini.
Kulingana na Rashid Omar ambaye aliongea kwa niaba ya wengine na ambaye amewahi kufanya kama kibarua katika shirika la bandari alisema kuwa ana imani na uongozi wa mwanamke iwapo atapewa nafasi ya kuongoza shirika hilo badala ya kuendelea kuwapa nafasi wanaume ambao tayari wameonyesha utepetevu katika kuendeleza shirika hilo ambalo huchangia kuinua uchumi wa nchi.
“Wanawake wakipewa nafasi wataleta nafuu katika mashirika yetu ambayo yametawaliwa na ufisadi kutokana na uongozi mbaya wa wanaume, hivyo tunamwomba Rais na waziri kuliangalia suala hilo kwa undani na kumpa mwanamke nafasi kuwa mkurugenzi mkuu,” alisema mkazi huyo.
Hata hivyo wengi wa wachanganuzi wa masuala ya Pwani wanasema kuwa huenda Catherine Wairi ambaye amewahi kuhudumu kama kaimu meneja na kuleta mabadiliko katika shiriko hilo kwenye mapato ya shirika hilo ambalo lilikuwa limekumbwa na hasara miaka kama mitano iliyopita.