Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Ikiwa imesalia siku moja kabla ya kuwasili kwa kiongozi wa kanisa katoliki duniani Baba Mtakatifu humu nchini, wakazi wa mjini Mombasa wamehimizwa kuungana na kuliombea taifa hili kuwa la amani.

Akiongea mjini Mombasa siku ya Jumatatu, kiongizi wa vijana katika eneo la Kisauni Maxwell Masai, alisema kwamba taifa hili linahitaji kuungana pamoja na kueneza ujumbe wa amani ili kuzuia misukosuko ya kiusalama inayolikumba.

Kulingana na Masai, iwapo wakenya, na hususan wakazi wa Mombasa watawajibikia swala hilo, basi changamoto taifa hili linapitia kwa kiwango kikubwa zitaisha na jamii itaishi kwa amani bila misukosuko yoyote ya kiusalama.

Masai amesema kwamba jamii inafaa kuwa katika mstari wa mbele kuwaonganza vijana katika kutambua umuhimu wa kudumisha amani kwa kiongozi anayetarajiwa kuwasili humu nchini ataleta manufaa kwa wakenya na ujumbe wake utaimarisha taifa hili kwa kiwango kikubwa.

“Tunawasihi vijana kutumia fursa hii kwa kupokea ujumbe wa Papa Francis wa amani na kusitisha visa vyote vya kihalifu na kudumisha amani ili taifa hili kuwa la muungano,” alisema Masai.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani anatarajiwa kuwasili humu nchini siku ya Jumatano na kufanya ibada maalum ya kueneza amani nchini na barani Afrika.