Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa Mombasa wamepinga kauli ya rais Uhuru Kenyatta ya kutaka kupelekwa kwa wanajeshi wa muungano wa AMISOM katika eneo la Gedo, Somalia.

Wakizungunza na mwanahabari huyo siku ya Jumapili, wakazi hao walisema kuwa raisi anafaa kukumbuka jinsi wanajeshi wa Kenya walivyouawa nchini Somalia wala si kusisitiza kupelekwa wanajeshi hao tena nchini humo.

Suleiman Ali, mkazi wa Buxton alisema kuwa haitakuwa vizuri kupeleka kikosi hicho ikizingatiwa ni hivi majuzi tu idadi ya wanajeshi wa Kenya walishambuliwa na kupoteza maisha wakiwa Somalia.

Hatua hii inajiri baada ya rais Kenyatta kutaka kupelekwa kwa haraka wanajeshi wa muungano wa AMISOM katika eneo la Gedo, akisema kuwa eneo hilo limekuwa ngome ya wapiganaji wa Al Shabaab nchini Somalia.

Akizungumza nchini Djibouti katika kongamano la mataifa yanayounda vikosi hivyo vya Amisom, Kenyatta alisema kuwa kukosekana kwa wanajeshi katika eneo hilo imesababisha wasi wasi mkubwa kwa taifa la Kenya.

Amehusisha shambulizi dhidi ya wanajeshi wa Kenya huko El Adde akisema ilikuwa jaribio la juhudi za mataifa hayo kuangamiza ugaidi.

Rais amesema lengo kuu ni kuleta usalama nchini Somalia kwa kuangamiza uwezo wa Alshabaab.

Ametaja changamoto inayokumba vikosio vya Amisom ni kutokuwa na uwezo wa kuwepo kila mahali katika taifa la Somalia hivyo basi kutoa fursa kwa al shabaab kutekeleza mashambulizi katika baadhi ya maeneo.