Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakazi Mombasa wameshauriwa kuwekeza pesa zao katika mashirika ya bima, kama njia mmoja wapo ya kuhifadhi pesa hizo kwa matumizi ya siku za usoni.

Akizungumza na wanahabari siku ya Jumanne katika hoteli moja mjini Mombasa, Mkurugenzi mkuu wa shirika la bima la Jubilee Insurance, David Ogega, aliwashauri wakazi kuwa na mazoea ya kuwekeza pesa zao.

Ogega alisema kuwa fedha zitakazowekezwa katika hazina ya mashirika ya bima zitasaidia pakubwa katika kuwafaidi wakazi wakati wa kustaafu.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa wakazi wengi wanasalia maskini kwa kutokuwa na akiba za matumizi hasa wanapostaafu.

Aidha, aliongeza kuwa kuwekeza ni njia moja wapo ya kuinua kiwango cha biashara nchini, na kuwahimiza wafanyikazi kujitahidi kuwekeza pesa zao katika mashirika ya bima.