Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakazi katika eneo la Njoro na viunga vyake wamewataka maafisa wa usalama kuimarisha doria sawia na kuchunguza wahalifu.

Wakazi hao walisema kuwa visa vya maafa ya kiholela vimeongezeka katika eneo hilo.

Haya yanajiri baada ya mtu mmoja kupatikana akiwa ameaga dunia baada ya kugongwa na shoka kichwani katika eneo la Bondeni viungani mwa jimbo ndogo la Njoro.

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatatu, wakazi hao, wakiongozwa na Kariuki Njau, walisema kuwa ipo haja hali ya usalama kuimarishwa katika eneo hilo hususan msimu huu wa likizo ambapo visa vya aina hiyo huongezeka.

Wakazi hao aidha wamewashawishi vijana kutojihusisha na vikundi vya uhalifu.

“Ningependa kuwasihi vijana wajiepushe na vikundi vya uhalifu katika eneo hili kwasababu mkiharibu usalama nanyi mtaishi vipi?” alisema Bw Kariuki.

Aliongeza, “Ikiwa tunataka eneo letu liendelee kimaendeleo, basi hatuna budi ila kushirikiana kuimarisha usalama. Haya magenge hayatatufaidi bali yatatumaliza.”