Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wizara ya barabara na ujenzi nchini imeombwa kuweka matuta na alama za barabarani kwenye barabara ya kutoka Kisii-Mbanda-Kegogi.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatano mjini Kisii, wakazi wa maeneo hayo waliomba idara husika kujali maisha ya wananchi kwa kuweka matuta kwa barabara hiyo ili kuwalazimisha madereva kuendesha gari kwa mwendo usio wa kasi.

Haya yanajiri siku moja baada ya mtoto kugongwa na gari alipokua akivuka barabara hiyo katika eneo la Nyatieko.

Wakazi hao wameomba hatua ya dharura kuchukuliwa ili kupunguza ajali hizo zinazoendelea kufanyika katika barabara hiyo kila kuchao.

“Ajali zimekuwa zikiongezeka katika barabara ya Kisii-Kegogi. Tunaomba kuwekewa matuta katika barabarani hiyo pamoja na alama za barabarani,” alisema Shem Ondari, mkazi.

Aidha, Charles Ong’era, mkazi mwingine alisema kuwa waendeshaji pikipiki hupita katika barabara hiyo kwa mwendo wa kasi na kuwepo kwa matuta kutasaidia katika kudhibiti hilo.

“Tunaomba maafisa wa trafiki kutusaidia kuweka vizuizi kwenye barabara hii kuyanasa magari yasiyo na vidhibiti mwendo, ili kupunguza visa hivi vya ajali za mara kwa mara,” alisema Ong’era.