Wakazi katika eneo la Mrima kaunti ya Mombasa wamewataka wachuuzi wote wa vyakula na hata wale wanaouza nyama kudumisha usafi wa hali ya juu kufuatia tangazo la hivi majuzi kuwa kunahofiwa mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Akiongea na mwandishi huyu, Agnes amesema kuwa hofu yake ni jinsi nyama inavyobebwa na kuongeza kuwa baadhi ya wauzaji wa mboga hiyo hawazingatii usafi kamwe.
Naye Asman amewataka wauzaji vinywaji kutumia maji safi yaliyotibiwa ili kuepuka maradhi hayo.
Licha ya visa vichache vya kuhara kuripotiwa katika hospitali ndogo ya eneo hilo, daktari amekanusha kuwa huenda ikawa kipindupindu.
Hata hivyo, wakazi wote wameombwa kudumisha usafi wa ndani na nje ya nyumba ili kuwa salama.