Wakazi wa Kivumbini, mjini Nakuru, wameipongeza serikali ya kaunti kwa kuzibua mitaro ya maji taka, huku wakisema shughuli hiyo ita imarisha hali ya usafi kwenya kitongoji hicho.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongea siku ya Jumapili na mwandishi huyu, wakazi hao walisema uchafu uliokua kwenye mitaro hiyo ulikua tishio kwa afya ya wakazi na wapita njia.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya wakazi hao kumlalamikia mwakilishi wao wa wadi Bwana Vitalis Otieno, kwa kusema kuwa kitongoji hicho kiko kwenya hatari ya kukumbwa na mafuriko iwapo mvua ya El Nino itanyesha kufuatia kuziba kwa mitaro.

Harron Ochieng, mkazi, alisema sasa hatari ya kukumbwa na mafuriko haiko tena

"Wakati wa mvua maji taka huingia katika nyumba zetu na kuleta tisho la magongwa, Tunashukuru serikali ya kaunti kwa kuzibua mitaro kwa vile sasa hatutashuhudia mafuriko katika eneo hili,” alisema Ochieng.

Wakazi hao sasa wameitaka serikali ya kaunti kuzibua mtaro unao pitisha maji taka kutoka eneo la Flamingo hadi Mbuga ya wanyama ya Nakuru.