Share news tips with us here at Hivisasa

Wakenya kote nchini wametakiwa kuiga mfano wa Waislamu waliyowakinga wenzao Wakristo dhidi ya kushambuliwa na wanamgambo wa al-Shabaab siku ya Jumatatu katika Kaunti ya Mandera.

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Alhamisi, mwenyekiti wa Chama cha Nakuru Abagusii Welfare Association (NAWA), George Omwanza, alisema isingelikuwa undugu na umoja wa abiria hao, kungekuwa na mashambulizi mabaya.

“Ingawa watu wawili waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa wakati wa tukio hilo, Wakenya walipata kujua kuwa amani, upendo na umoja ndizo nguzo za nchi,” alisema Omwanza.

Mwenyekiti huyo alipendekeza kufutilia mbali migawanyiko kwa misingi ya kikabila, kisiasa kwa kusema athari zake zitakwamisha na kurudisha nyuma maendeleo.

Omwanza alisema upendo na umoja wafaa kuanza kudhihirishwa wakati huu wa krismami na mwaka mpya na hata katika siku za usoni.

Matamshi haya yanajiri baada ya miito sawia kuendelea kutolewa kote nchini ikipongeza hatua ya abiria hao waliyowakinga wenzao dhidi ya shambulizi hilo.