Share news tips with us here at Hivisasa

Wakristo wametakiwa kuwajali wajane na mayatima.

 Wito huo ulitolewa na Padre Francis Muriithi wa kanisa katoliki Nakuru ambaye alisema kuwa kuna umuhimu wa makundi sahaulika kukumbukwa.

"Kama jamii ni vyema tuonyeshe upendo kwa wote na hasa wajane na yatima"alisema Muriithi.

Wakati huo huo, alitoa wito kwa wakristo kuliombea taifa tunapokaribia uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.