Share news tips with us here at Hivisasa

Baadhi ya wakulima kutoka wodi ya Gesima wamejitokeza kuiomba serikali ya kaunti ya Nyamira kukumbatia teknolojia yakisasa ili kuimarisha kilimo cha uzalishaji katika kaunti hiyo.

Wakulima hao wakiongozwa na msemaji wao Florence Machoka wamesema kuwa serikali ya kaunti hiyo inafaa kuwapa vyandarua wakulima ili viwasaidie kukuza mimea na mboga mbalimbali na pia iwape hamasa wakulima ya jinsi yakutumia teknolojia hiyo mpya ili kuimarisha maisha yao ya kila siku.

"Sisi kama wakulima tunaiomba serikali ya kaunti ya Nyamira kupitia kwa wizara ya kilimo kuhakikisha kuwa tumepokezwa vyandarua vyakukuza mimea mbalimbali na pia kutupa mafunzo ya jinsi yakutumia vyandarua hivyo ili kuimarisha mapato yetu na tunataka serikali ya kaunti hii iige mfano wa kaunti zingine kama vile ya Kisii ili kukumbatia teknolojia wanazozitumia wakulima hao," Alisema Machoka. 

Kwa upande wake mkaazi mmoja wa eneo hilo anayekuza viazi Edward Moseti alisema kuwa uchumi wa mataifa yanayoendelea kustawi huimarika kutokana na kilimo na akaiomba serikali ya kaunti hiyo kuekeza zaidi kwenye kilimo ili kuimarisha uchumi.

"Mataifa yanayostawi hutegemea sana kilimo endelevu naningependa kuisihi serikali ya kaunti hii kuekeza pakubwa kwenye kilimo ili kustawisha uchumi wake," alihoji Moseti.