Mwenyekiti katika kiwanda cha majani chai cha Kebirigo David Kireri amewashauri wakulima wa zao hilo katika kaunti za Kisii na Nyamira kuuzia halmashauri ya majani (KTDA) mazao yao ili kunufaika zaidi.
Kulingana naye, wakati wakulima huuza zao hilo kwa kampuni tofauti hawawezi kunufaika na pesa zile za ziada ilimaarufu kama ‘bonus’ baada ya mwaka kukamilika na kusema hiyo ni hasara kubwa.
Wakulima hao sasa wametakiwa kupanua na kuboresha kilimo hicho kwa kupeleka mazao yao kwenye vituo vya halmashauri hiyo ya KTDA ambapo watalipwa vizuri na kwa wakati unaofaa.
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya jumatatu mjini Nyamira, Kireri alisema kuwa wakulima hao mara nyingi hunyanyaswa na malanguzi au madalali wa majani chai ambao huchukua zao la wakulima wakiahidi kuwalipa pesa na baadaye na hutoroka au wanapopima uzani wanawanyanyaza kwa kutumia vipimio ambavyo haramu.
“Naomba kila mkulima wa majani chai kuimarisha kilimo cha chai katika kaunti za Nyamira na Kisii ili kujinufaisha zaidi,” alisema mwenyekiti huyo.
Wakati huo huo, Kireri aliahidi kuwasaidia wakulima ili kupeleka majani chai yao kwa halmashauri ya KTDA ili kunufaika kupitia upanuzi wakilimo cha mumea huo.