Walimu 12 wa shule ya msingi ya Star of The Sea wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa mitihani.
Mahakama ilielezwa kuwa Novemba 10, 2015 walimu hao wanadaiwa kupatikana na mitihani ya masomo ya hesabati na kiingereza katika shule hiyo.
Walimu hao walikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Diana Mochache.
Mahakama iliwaachilia kwa dhamana ya Sh500,000 ama Sh200,000 pesa taslimu kila mmoja.
Akitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi, Hakimu Mochache alisema kuwa hatua hiyo itakuwa funzo kwa wengine watakao patikana na makosa ya udanganyifu wa mitihani nchini.
Hakimu huyo alisema kesi hiyo itasikizwa Disemba 14 na 16 kabla ya matokeo ya mitihani mwakani, mashahidi wanane watakapotoa ushahidi wao.