Mwaniaji wa Ubunge kutoka eneo bunge la Borabu Nyandoro Kambi amewataka walimu kuweka mikakati ya kuimarisha viwango vya elimu katika eneo la Borabu ili kusaidia katika kuinua viwango vya elimu katika eneo eneo hilo.
Akihutubu katika shule ya msingi ya Matongo siku ya jumatatu alipopokeza shule hiyo vitabu vya kusoma Nyandoro alisema kuwa, viwango vya elimu katika eneo hilo vitaimarika iwapo walimu watajitolea kuwahudumia wanafunzi vilivyo huku akiwahimiza maafisa wa elimu na walimu wakuu wa shule kuhakikisha kuwa walimu wote wanahudhuria vipindi vyao darasani inavyohitajika.
"Sharti walimu wetu wajitolee kuwahudumia wanafunzi iwapo tunataka kuimarisha viwango vya elimu katika shule zote za eneo hili na suala la baadhi ya walimu kutohudhuria madarasani inavyohitajika sharti lishughulikiwe kiukamilifu," Alisema Kambi.
Kambi alisistiza kuwa Wakfu wa Nyandoro Kambi utaendelea kusaidia kufadhili shule mbalimbali huku akiwahimiza walimu kujitolea kuhakikisha kuwa wanatumia vitabu alivyopokeza shule hiyo ili kuwaanda vyema wanafunzi kwa mitihani ya kitaifa.
"Wakfu wa Nyandoro Kambi utahakikisha kuwa unasaidia shule mbalimbali huku Nyamira ili kuimarika kimasomo na tunalohitaji kuona kuimarika kwa viwango vya elimu nikujitolea kwa walimu wetu," Alisema Kambi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa muungano wa walimu na wazazi katika shule hiyo Kennedy Mogire alishkuru kambi kwa ufadhili wa vitabu huku akiongezea kwa kutoa ahadi zakuhakikisha kuwa wazazi na walimu wameshirikiana ili kuimarisha viwango vya elimu katika shule hiyo.
"Kwa kweli tumefurahi kupokea ufadhili huu wa vitabu kutoka kwa Wakfu wa Nyandoro Kambi na tunaahidi kuwa sisi kama wazazi tutashirikiana na walimu ili kuhakikisha kuwa tunaimarisha viwango vya elimu ili tuwe na matokeo mema kwenye mitihani ya kitaifa," alisema Mogire.