Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mshirikishi wa mashirika ya kijamii ya Dzarino, Lizzie Okwaro, ameshinikiza wamiliki wa nyumba za kukodisha katika Kaunti ya Mombasa kuzingatia usafi, ili kuzuia mkurupuko wa magojwa yanayayosababishwa na uchafu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Aldina eneo bunge la Jomvu Kuu, siku ya Ijumaa, Okwaro alisema kuwa sharti wamiliki hao washinikize usafi wa mazigira miongoni mwa wapangaji wao, ili kuhakikisha usafi katika jamii.

Aidha, ameitaka jamii kushirikiana na makundi ya vijana wanaobeba taka katika maeneo mbali mbali, ili kuhakikisha mazingira masafi katika maeneo ya Pwani.

Kulingana na Okwaro, usafi wa mazingira utawezesha wakaazi kuishi katika makao safi haswa wakaazi wa maeneo ya Kilindini na Likoni, yaliyo na idadi kubwa ya wanaougua Ukimwi, ili kupunguza makali ya kuenea kwa magojwa ibuka kwa waathiriwa, kwasababu ya ukosefu wa kinga mwilini.

Vilevile,  kiongozi wa kundi la vijana la kuzoa taka cha Kuzola Esther Nyamvula, alitoa wito kwa wamiliki wa nyumba kujisajili katika orodha za nyumba zilizosajiliwa kubebewa taka kwa ada ya chini, ili kudumisha usafi katika maeneo mbali mbali .

Nyamvula alisema kuwa idadi kubwa ya wakaazi wa eneo la Aldina, eneo bunge la Jomvu Kuu, wanaishi katika nyumba za kukodisha zilizo na mazingira machafu kwa kutozingatia kanuni za usafi.

Alisema kuwa hali hiyo husababisha kuenea kwa magojwa mbali mbali haswa kipindupindu.