Wanachama 42 wa Mombasa Republican Council (MRC) walikokuwa wanakabiliwa na madai ya kuandaa mkutano bila kibali waachiliwa kwa dhamana ya shilingi 200,000 kila mmoja.
Akitoa dhamana hiyo siku ya Ijumaa, Hakimu mkaazi Paul Mutai, aliwaagiza washukiwa hao kulipa dhamana hiyo na mdahamini wa kiasi sawa na hicho, la sivyo kusalia rumande hadi kesi inayowakabili kutamatika.
42 hao wakiwemo wanawake wasita walitiwa nguvuni mnamo Desemba 31, 2015 katika eneo la Tiwi eneo bunge la Matuga.
Aidha, washukiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kuandaa mkutano kinyume cha sheria, kuwa wanachama wa kundi lililopigwa marufuku pamoja na kuchangisha pesa za jumla ya shilingi 67, 150 kinyume cha sheria.
Kesi yao inatarajiwa kutajwa tarehe Januari 22, 2016 na kusikilizwa Machi 21, 2016.