Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanachama wanne wa vuguvugu la MRC wanaokabiliwa na kosa la mauaji na kuzua vurugu wakati wa uchaguzi wa mwaka 2013 watajua hatma yao tarehe Machi 13, 2016.

Hii baada ya mahakama kuu ya Mombasa kuwapata na makosa ya mauaji ya mlinzi wa Gavana wa Kilifi Amason Kingi.

Wanne hao, Faraji Konde Kazungu, Omari Diofu Gwashe, Suleiman Mohamed Suleiman na Justus Randu Nyando, wanakabiliwa na madai ya mauaji ya askari Harrison Maitha, aliyekuwa mlinzi wa Gavana wa Kaunti ya Kilifi Amason Kingi mnamo Octoba 4, 2012 katika eneo la Mtomondoni huko Kilifi.

Aidha, wanne hao wanakabiliwa na kosa la kupanga njama ya kuvuruga uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 huko Kilifi.

Vile vile, wanakabiliwa na shtaka la kupanga njama ya kuvuruga mtihani wa kitaifa wa mwaka 2013 huko Kilifi.