Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanafunzi waliokamilisha darasa la nane wameonywa dhidi ya kusherekea matokeo yao ya mitihani wa KCPE katika sehemu za burudani. 

Akizungumza alhamisi ofisini mwake, chifu wa Solai bwana Simon Murage amewaonya wanafunzi hao dhidi ya kutangamana kwenye sehemu za burudani kwani wanatahadharisha maisha yao. 

"Tunawaonya wanafunzi waliopata matokeo yao kutoenda kwenye vilabu, sinema na sehemu zinginezo kwani wanaweza kulaghaiwa na kujikuta pabaya kwani sehemu nyingi kama hizi kuna madawa ya kulevya na mihadarati," amedokeza Murage.

Aliongeza kuwa watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria huku akiwaonya dhidi ya kurandaranda nyakati za usiku. 

Chifu huyo amechukua fursa hiyo kuwaomba wazazi kuwa makini na wanao huku akiwataka kuwapa ushauri ili kuwatayarisha kukumbana na changamoto watakazo kumbana nazo.