Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ufundi cha Mombasa (TUM) wamelalamikia utovu wa usalama katika maeneo yanayozingira.
Wanafunzi hao wamesema kuwa wengi wao wamepoteza vitu muhimu kama vile simu, vipatakalishi na hata kupoteza maisha yao mikononi mwa wahalifu.
Mwakilishi wa wanafunzi Ben Nganga amesema kuwa kuna wahuni ambao huwaangaisha wanafunzi hao na wengi wao huishi karibu na lori za kubeba taka zilizoko karibu na chuo hicho.
“Tungependa kutoa wito kwa maafisa wa usalama kushirikiana nasi ili tuweze kukomesha wahuni hawa ambao wanatudunga visu,” alisema Nganga.
Kwa sasa wanafunzi hao wamekuwa wakiishi kwa hofu baada ya wengi wao kukabiliwa na wahalifu hao na wameapa kuwa iwapo serikali haitachukua hatua ya kuhakikisha usalama wao basi wenyewe watachukua juhudi za kuwasaka.