Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu wameonywa dhidi ya kuingilia maswala ya kisiasa, na badala yake kutakiwa kuangazia na kutetea masilihi muhimu yanayomuathiri mwananchi.

Kauli hio ilitolewa siku ya Jumapili na mwakilishi wadi ya Kadzandani Mohamed Ndanda kwenye kikao na wanahabari katika hoteli moja mjini Mombasa.

Ndanda aliwataka wanaharakati hao kushughulikia maswala kama vile ya ardhi,ufujaji wa fedha na mihadharati na kukoma kuchafua majina ya wanasiasa kwa maswala yasiyokuwa na msingi.

Aidha, alidai kuwa baadhi ya wanaharakati wanatumiwa kisiasa ili kuwapaka matope baadhi ya viongozi jijini Mombasa.politics