Makundi ya wanaharakati kutoka mjini Naivasha yameteta vikali kutokana na jaribio la unyakuzi wa kipande kimoja cha ardhi ya umma mjini humo, karibu na jengo la Jubilee.
Wanaharakati hao wamedai kuwa baadhi ya maafisaa walio na usemi mkubwa serikalini wameanza kunyakua ardhi hiyo na ambayo hutumiwa kama bustani ya umma ili kujifaidi wenyewe.
Makundi hayo sasa yameapa kuelekea mahakamani ili kupinga hatua zozote za kubinafsisha ardhi hiyo inayotumiwa na wakaazi wengi.
Mmoja wao Benjamin Muungania amesema kuwa wafanyibiashara aghai wanataka kutumia ardhi hiyo kibiashara, hatua ambayo ni kinyume cha sheria.
Muungania amesema kwa sasa wanazuilia unyakuzi huo kwa kupanda miti kwenye kipande hicho cha ardhi.
"Kando na ardhi hiyo kutumiwa na wakaazi kama bustani ya kupumzikia, pia hutumiwa kila wakati ambapo kuna uchaguzi kama kituo cha kupigia kura" akasema Muungania.