Wananchi wametakiwa kutembelea madaktari wa meno ili kuzuia athari za magonjwa ya meno.
Wataalamu hao wa meno nchini wamewataka wananchi kutembelea vituo vya meno angalau mara moja kwa mwaka kwa ajili ya kuzuia athari za magonjwa ya meno.
Mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha madaktari wa meno, wa tawi la Pwani Daktari Evelyn Sumbi, siku ya Jumamosi, alisema ni jambo la busara kwa watu kujua afya yao ya meno ili kuepuka maradhi ya hatari kama saratani.
Maafisa hao wameyasema haya siku ya Jumamosi, mjini Mombasa wakati wa sherehe ya kuadhimisha usafi wa meno duniani iliyodhaminiwa na chama cha madaktari wa meno.
Sherehe hiyo iliwajumuisha wanafunzi na waalimu kutoka shule mbali mbali kutoka Mombasa waliofunzwa jinsi ya kutunza meno yao ili kujiepusha na magonjwa mbali mbali ikiwemo saratani ya mdomo.