Share news tips with us here at Hivisasa

Wananchi wa Malindi wametakiwa kutokubali kugawanywa kwa misingi ya kisiasa na kikabila.

Kauli hii ilitolewa na mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir alipokuwa akihutubia wananchi huko Malindi.

Nassir, amewataka wananchi hao kuzingatia maadili mema na juhudi za kiongozi watakaye mchagua.

“Ukombozi kwa wakaazi wa Malindi utapatikana iwapo mjumbe atakayechaguliwa ataweza kuyatetea maslahi ya wakaazi,” alisema Nassir.

Aliwaonya wananchi kutotumiwa vibaya na watu wenye malengo ya kibinafsi, sawa na kutokubali kugawanywa kwa misingi mbalimbali, akisema endapo wataruhusu hilo, basi kuna hatari ya kupatikana kwa kiongozi asiyefaa.

Nassir anampigia debe mjumbe wa chama cha ODM, akisema kwamba tayari muungano wa Jubilee hauna nia ya kuwatetea wananchi, akisema hili linadhihirika katika upitishwaji wa sheria kandamizi.