Daktari Stanley Chege Karanja ambaye ametangaza rasmi kuwa atawania kiti cha ubunge cha Nakuru mjini mashariki mwaka wa 2017 ametoa wito kwa wananchi kuepuka na siasa potovu za mgawanyiko.
Akizungumza mjini Nakuru, Karanja alisema kuwa wakati ni sasa wa viongozi kupigwa msasa kabla ya kuchaguliwa mwaka wa 2017.
"Wananchi munafaa kuwachunguza viongozi kabla ya kuwachagua,"alisema Karanja.
Kwa mujibu wake, wakati wa siasa potovu za ukabila na vita ushapita na sasa ni wakati wa siasa za amani na maendeleo.
Akigusia matokeo ya mtihani wa darasa la nane ya mwaka huu yaliyotangazwa jumatano na waziri wa elimu Dr Fred Matinag'i, Karanja aliwapongeza wale wote waliofanya vyema.
Wakati huo huo, aliunga mkono usemi wa waziri Matiang'i kwamba swala la udanganyifu wa mitihani linafaa kushughulikiwa haraka iwezekanavyo.