Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Huku Wakenya wakijiandaa kumpokea Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, Idara ya usalama katika Kaunti ya Mombasa imewahikishia waumini wa dini ya Katoliki wanaosafiri kuelekia jijini Nairobi usalama dhabiti.

Akizungumza afisini mwake mjini Mombasa siku ya Jumanne, Naibu Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Salim Mahmoud alisema kwamba serikali imejiandaaa vilivyo kuimarisha usalama kuanzia kaunti ya Mombasa hadi jijini Nairobi.

Mahmoud alisema kwamba tayari vikosi maalum vya kupambana na wahalifu vimepangwa kuambatana na msafara huo huko jijini Nairobi na akawaonya wanaopanga njama ya kuvuruga msafara huo kuwa watakabilia kikamilifu.

“Tunawahakikishia waumini wa dini ya katoliki wanaosafiri kushiriki ibada ya Papa Francis usalama wakutosha. Wanaolenga kuvuruga msafara huo wafahamu kuwa maafisa wa polisi watawakabili kisheria,” alisema Mahamoud.

Wakati uo huo Naibu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mombasa Padri Wilbard Lagho aliwataka wakazi wa Kaunti ya Mombasa na Pwani kwa jumla kuliombea taifa hili kuepukana na changamoto linazopitia ili jamii kuishi kwa amani.

Zaidi ya waumini 900 wa Kanisa Katoliki wameanza msafara huo kueleka jijini Nairobi na kukita kambi katika maeneo ya Macknon road, Voi, Makindu na Machakos wakieneza ujumbe wa amani kabla ya kujumuika na waumini wengine katika ibaba hiyo maalum itayoongozwa na Papa Francis.