Wanawake mjini Mombasa wamehimizwa kugombea na kuwania nafasi za uongozi katika serikali ili kuongeza idadi ya wanawake wanaoshikilia nyadhifa za juu serikalini.
Akihutubia wanawake katika eneo la Freretown siku ya Ijumaa, wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake, msimamizi wa Shirika la Actionaid Kenya kitengo cha haki za wanawake Kaunti ya Mombasa Caroline Nkirote, alisema kuwa wanawake huwa hawapati maendeleo kutokana na idadi yao ndogo serikalini.
Aliongeza kuwa iwapo idadi ya wanawake itaongezeka katika nyadhifa mbalimbali za uongozi, basi matatizo yao yatashughulikiwa kwa urahisi.
Nkirote amewataka kinamama wajihusishe katika masuala ya uongozi kupitia kuchaguliwa na wananchi na sio tu kuteuliwa na vyama.