Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wanawake wajawazito katika kaunti ya Kisii wameshauriwa kufika katika hospitali kupimwa na kujua hali zao za ugonjwa wa Ukimwi.

Hii ni baada ya kubainika kuwa idadi nyingi ya wanawake wajawazito hawaendi hospitalini kupimwa ugonjwa wa Ukimwi jambo ambalo limepelekea watoto wengi kuambukizwa ugonjwa wa Ukimwi

Akizungumza siku ya Jumapili katika hospitali ya rufaa na mafunzo mjini Kisii, mkurugenzi wa sekta ya afya katika kaunti ya kisii Daktari Geoffrey Ontomu aliomba wanawake wajawazito kuhakikisha wamepimwa ugonjwa wa Ukimwi.

Kulingana na Ontomu mazoea hayo ya kupimwa yatakupunguza maambukizi ya ugonjwa huo kwa wanao kwani watakabidhiwa dawa fulani ambao hupunguza maambukizi hayo mtoto anapokuwa bado hajazaliwa.

Kulingana na Ontomu mwanamke akibainika kuwa na virusi hivyo huwekwa kwa ratba ya kupokea dawa Fulani hadi ajifungue na kuelezwa jinsi ya kumlea mtoto kwa miaka miwili pasi kuadhirika na maambukizi ya Ukimwi.

“Mwanamke akifuata ushauri wetu na kunywa dawa husika, mtoto hawezi kupata ugonjwa wa Ukimwi," alisema Ontomu.

"Na anastahili kumnyonyesha mwiezi sita bila chakula chochote,” aliongeza Ontomu.