Wanawake na watoto wameombwa kuzingatia maagizo wanaposubiri kuabiri feri na wasimamizi wa shirika hilo.
Tangazo hili ni kufuatia malalamishi kutoka kwa walinzi wa Guardforce ambao wamekuwa wakipata wakati mgumu kuelekeza wanawake kutumia banda lao.
Akiongea na mwandishi huyu, mmoja wa walinzi hao alisema kuwa wanapata kazi ngumu kuwaongoza wengi wa wanawake na watoto, na kuwataka kuzingatia sheria.
"Wanawake hao hukimbilia banda la wanaume na huko msukumano huwa hatari kwani hawajali. Wengine na watoto wachanga utawakuta wakibana kupenyeza humo," aliendelea mlinzi huyo.
Aidha aliongezea kuwa hata visa vingi vya utovu wa nidhamu wanavyofanyiwa wanawake hapo ferini si vya kujitakia.
"Mwanamke amevaa vazi la kubana ajabu halafu anajisunda kwa wanaume, watarajia nini," aliuliza.
Watu wote kwa jumla wameombwa kutilia maanani masharti yaliyowekwa kwa uendeshaji mzuri wa shughuli za wote.