Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Msimamizi wa kijinsia katika Chuo Kikuu cha Kisii kilichoko, Callen Nyamwange amewashauri wanawake kusoma katiba kubaini haki zao ili kujipigania katika jamii.

Ushauri huo umetolewa baada ya kubainika kuwa idadi nyingi ya wanawake wanasumbuliwa na wazee wao na ata kutelekezwa katika jamii huku wakionekana kutokuwa na haki ya kujipigania.

Akihutubia wanawake na wanafunzi wa shule za sekondari mjini Kisii, Nyamwange aliomba wanawake kusoma katiba kujua haki zao ili wasidhulumiwe haki zao katika jamii.

“Kile ambacho kimechangia wanawake kusumbuliwa katika jamii ni kutojua haki zao. Kila mwanamke anastahili kusoma katiba kujua haki zake,” alisema Nyamwange.

Wakati huo huo, Nyamwange aliwahimiza wazee katika jamii ya Kisii kushirikiana na wanawake kwa kuwaunga mikono wanawake katika kuwania nyadhifa mbalimbali za kisiasa huku akisema wanawake wanastahili kuwa viongozi kulingana na katiba.

“Naomba wazee kushirikiana na wanawake wanapowania viti mbalimbali vya uongozi kwani wote wanaruhusiwa kuwa viongozi humu chini,” aliongeza Nyamwange

Matamshi yake yaliungwa mkono na mwandishi wa vitabu Peter Questt ambaye alisema wanawake wako na nafasi ya kuwania viti vya uongozi nchini na kuwashauri kuto ogopa kukutana uwanjani na wazee kupambana kisiasa.