Afisa wa elimu katika kaunti ya Kisii Henry Onderi amewaomba washikadau wote wa elimu katika kaunti hiyo kushirikiana na waziri wa elimu nchini Fred Matiang’i kupambana na kupunguza visa vya udanganyifu wa mitihani nchini.
Ombi hilo limetolewa baada ya waziri Matiang’i kuomba ushirikino kupunguza visa hivyo vya wizi wa mitihani, jambo ambalo si la kufurahisha wakati wanafunzi wanakosa kupata majibu ya mitihani kila mwaka.
Akizungumza siku yaJumanne mjini Kisii, Onderi alisema ikiwa visa hivyo vya wizi wa mtihani vitapunguzwa, sharti ushirikiano wa washkadau uwe ili nchi iokolewa kutoka udanganyifu wa mitihani.
“Naomba wazazi, bodi za shule, walimu na wanafunzi kushirikiana pamoja kuhakikisha udanganyifu wa mitihani umekomezwa nchini,” alisema Onderi.
“Wizi katika mitihani umekuwa donda kwa wengi ambapo wengi hukosa majibu ya mitihani yao, jambo ambalo hurudisha masomo nyuma kwa wale wanahusika kwa visa hivyo,” aliongeza Onderi.
Onderi alimhakikishia waziri Matiangi kuwa atashirikiana naye kupunguza visa hivyo vya mtihani haswa katika kaunti ya Kisii.
Wanafunzi zaidi ya 5,000 walihusishwa katika visa vya udanganyifu mwaka jana huku waziri Matiang'i akitangaza wanafunzi hao kuchukuliwa hatua kando na shule jinsi ilivyokuwa hapo awali.