Share news tips with us here at Hivisasa

Washukiwa wawili wa ulanguzi wa pembe za kifaru wametozwa dhamana ya shilingi milioni 10 kila mmoja.

Washukiwa hao, Ali Omar Haji na Said Alfani Mwinyi wanadaiwa kupatikana na pembe za kifaru zenye thamani ya shilingi milioni 3 mnamo Disemba 27, 2015 katika eneo la Mama Ngina.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatano, hakimu Diana Mochahce alisema kuwa hakuona sababu mwafaka zilizotolewa na upande wa mashtaka za kuwanyima dhamana wawili hao.

Aidha, amepuzilia mbali madai ya kuwahusisha washukiwa hao na ugaidi na ulanguzi wa dawa za kulevya kama inavyodaiwa na upande wa mashtaka ikizingatiwa kuwa hadi sasa hakuna ripoti yoyote kutoka kwa maafisa wa  ATPU inayowahusisha na ugaidi.

Kesi yao itatajwa Februari 24, 2016.