Share news tips with us here at Hivisasa

Washukiwa wawili wa ugaidi watasalia korokoroni kwa siku 30 kusubiri uchunguzi dhidi yao kukamilika.

Hii ni baada ya afisa wa upelelezi Gabriel Karuguh kuwasilisha ombi mahakamani siku ya Alhamisi la kutaka kupewa muda zaidi wa kukamilisha uchunguzi wake.

Karuguh aliambia mahakama kuwa wawili hao, Mohamed Ali Saudi na Abdallah Ali waliokamatwa siku ya Jumatano katika eneo la Malindi, wanadaiwa kuhusishwa kuwa na ukaribu na kundi la wanamgambo la al-Shabaab na kutoa makaazi kwa magaidi hao.

Aidha, aliongeza kuwa wawili hao wanadaiwa kuwa na uhusiano na wale waliokwepa mtego wa polisi katika eneo la Majengo.

Hakimu katika mahakama ya Mombasa, Diana Mochache alikubali ombi hilo na kuagiza kuzuiliwa kwa wawili hao katika Kituo cha polisi cha Makupa.