Maafisa wa polisi mjini Mombasa wanawazuilia washukiwa wawili wa ugaidi waliyotia nguvuni katika eneo la Majengo mjini Mombasa siku ya Ijumaa wakiwa na njama ya kutekeleza ugaidi hapo jana.
Mohammed Salim na Mohammed Kombo waliotiwa nguvuni wanashukiwa kuwa ni wanachama wa mtandao wa magaidi waliyokuwa wakisakwa na maafisa wa polisi hapa Pwani.
Kulingana na maafisa wa kitengo cha kupambana na ugaidi, wawili hao wamehusika katika visa mbali mbali vya ugaidi katika Kaunti ya Mombasa na kwingineko Pwani.
Tayari Maafisa wa polisi wamepata idhini ya mahakama ya kuwazuilia washukiwa hao kwa siku 10 ili wakamilishe uchunguzi wao.
Afisa Mkuu wa polisi kisiwani Mombasa Martin Asin alithibitisha kuhusu kukamatwa kwa wawili hao.
Alisema kuwa baada ya kukamilisha kwa uchunguzi huo washukiwa hao wa ugaidi watawasilishwa mahakamani kufunguliwa mashtaka.
"Tumewakata washukiwa wawili wa ugaidi na tunawazuilia mpaka tukamilishe uchunguzi wetu na watafunguliwa mashtka na tayari maafisa wa polisi wanawasaka magaidi wengine wanajifucha na hivyo karibu watakamatwa," alisema Asin.