Washukiwa wawili wa wizi wametiwa mbaroni mjini kisii wakiwa na bidhaa mbalimbali vya wizi baada ya kufuatwa unyo kwa unyo na maafisa wa polisi.
Hii ni baada ya wananchi kupiga ripoti kwa maafisa hao wa polisi mjini Kisii jinsi wamekuwa wakiibiwa bidhaa zao na nyumba zao kuvunjwa kila wakati huku nyingi za nyumba hizo zikiwa zile za kupangisha
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kisii siku ya Jumanne baada ya shughuli ya kuwatia mbaroni wezi hao mkuu wa polisi wilayani Kisii ya Kati Francis Nguli alisema washukiwa hao wawili walitiwa mbaroni siku ya Jumamnne baada ya maafisa wa polisi kufanya msako na kuwatia mbaroni
Kulingana na mkuu huyo wa polisi, walifanikiwa kuvinasa bidhaa hivyo, vingi ni vya kutoka upande wa Egesa na eneo la Etago.
“Tuliwatia mbaroni washukiwa wawili wa wizi wakiwa na bidhaa vingi vya wizi, na sasa watafikishwa kortini kueleza kwa nini wanawasumbua wananchi kwa kuwaibia bidha zao,” alisema Francis Nguli, mkuu wa polisi wilayani Kisii ya kati.
“Tuliweza kuwatafuta washukiwa hawa baada ya kupokea ripoti zao kutoka kwa wananchi, wengi wao wakiwa wapangaji mjini humu na wamekuwa wakiibiwa sana na tutajaribu kuhakikisha wizi umekomeshwa,” aliongezea.
Aidha, Nguli aliomba yeyote amewai kuibiwa kufika katika kituo cha polisi cha Kisii ili kuona bidhaa vilivyonaswa kama ni miongoni mwa bidhaa walivyobiwa
“Naomba watu kutonunua bidhaa ambavyo si vipya kwani ukifumaniwa utahusika kama mwizi,” Nguli aliwaonya wananchi.