Share news tips with us here at Hivisasa

Wasichana wamehimizwa kuzingatia masomo wanayofundishwa shuleni ili kupata elimu bora.

Akizungumza siku ya Jumatatu, Mwenyekiti wa shirika la Maendeleo ya Wanawake katika Kaunti ya Mombasa, Afiya Rama, alisema wanawake wamesaulika katika nyanja ya elimu, hivyo basi kusisitiza kuwa ni sharti wasichana wajizatiti masomoni hasa ikizingatiwa kuwa elimu ndio msingi wa maisha bora.

Rama alisistiza haja ya kuzingatia umuhimu wa elimu katika nyanja mbalimbali huku akitaja siasa kama kigezo muhimu cha kugombea nyadhifa za uongozi.

Aidha, amewataka wanawake wanaonuia kuingia uongozini kujitoa kikamilifu ili kupata nyadhifa zilizoko.

Vilevile, amewataka wanawake kutambua haki zao za kimsingi katika nyadhifa kuu serikalini.