Wanafunzi wa shule ya kibinafsi ya Mt Sinai, iliyoko katika eneo la Likoni katika Kaunti ya Mombasa, walishikwa na mchecheto wakifanya mtihani wao baada ya mwanafunzi mwenzao kuwa mgonjwa ghafla baada ya kumaliza karatasi ya Kingeereza.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanafunzi huyo ambaye alianza mtihani wake vizuri siku ya Jumanne alisababisha hofu alipoanza kulia kwa machungu alipokuwa akimalizia karatasi ya pili ya siku ya kwanza siku ya Jumanne.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Paul Tawai, mwanafunzi huyo alikuwa mwenye furaha alipoanza karatasi yake mapema Jumanne asubuhi, lakini baada ya kuelekea kumaliza karatasi ya pili alionekana kutotulia na kuanza kulia huku akijishika kifuani.

Bwana Tawai alisema kuwa walilazimika kumpeleka kwenye kituo kimoja cha afya kilichoko karibu, ambapo alipata matibabu na kurejea kufanya karatasi ya mwisho ya siku hiyo lakini mambo yaliendelea kuwa mabaya zaidi baada ya mwanafunzi huyo kuanza kulia kwa machungu zaidi alipomaliza karatasi la pili la kiingegreza, hali ambayo ilishangaza wanafunzi pamoja na walimu na kuwabidi kumrudisha hospitali ili kupata matibabu maalum.

Mwalimu mkuu huyo alimtaja mwanafunzi huyo kuwa mwerevu na kiranja wa maswala ya michezo katika shule hiyo, na kuongeza kuwa kidogo hali hiyo iliwachelewesha lakini wanaamini mtihani huo utaendelea vizuri.

Kwenye mahojiano siku ya Jumatano, mwalimu alithibitisha kuwa mwanafunzi huyo amefanyiwa matibabu na ameingia darasani na kufanya mtihani wake.