Watu watano walifariki papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wameabiri kuhusika katika ajali ya barabarani katika eneo la Bonje kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi.
Akithibitisha ajali hiyo afisa mkuu wa trafiki eneo la Koleleni Rabai Francis Kibore alisema kuwa gari ya abiria aina ya Nissan na Lori ziligongana ana kwa ana na kusababisha ajali hiyo.
“Ajali hiyo ilitokea mwendo wa asubuhi baada ya lori kupoteza muelekea na kugongana ana kwa ana na garin hilo la abiria”, alisema Kibre siku ya Jumamosi katika eneo la ajali hiyo.
Kibore aliwatahadharisha madereva wa magari ya uchukuzi wa umma na yale ya kibinafsi kuwa waangalifu barabarani ili kuzuia kushughudiwa kwa ajali za mara kwa mara.