Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Shughuli za kawaida zimekatizwa katika eneo la Likoni, baada ya muungano wa wavuvi eneo hilo kuandamana wakilalamikia kutolipwa fidia na serikali baada ya kuharibu maeneo yao ya kuvua samaki katika bahari hindi ya Pwani.

Kulingana na Mwenyetikiti wa Muungano huo Kelly Konde, shughuli za uvuvi zilikatizwa baada ya serikali kuruhusu kampuni ya Wachina ya kujenga barabara ya Reli ya kisasa kutumia eneo la hilo kuchimba mchanga.

Akiongea na wanahabari katika maandamano hayo siku ya Ijumaa, Konde amesema kuwa serikali iliwaahidi kuwa kampuni hiyo ya wachina itawalipa fidia wavuvi hao lakini cha kustaajabisha hadi kufikia sasa hawajalipwa fidia hiyo na akiitaka serikali kuingilia kati na kutatua mzozo huo.

"Tunaitaka serikali kuingilia kati suala hili na kutulipa fidia maana tayari eneo hilo ambalo tunatumia kuvua samaki limeharibiwa na hatua hiyo imechangia pakubwa uharibifu wa mazingira," alisema Konde.

Amesema kuwa ujenzi huo umeharibu na kuathiri uzalishaji wa samaki kutokana na kuenea kwa vumbi la mchanga huo na kuvuruga maeneo yao ya kuvua samaki katika bahari hindi ya Pwani.

Kauli ya kiongozi huyo wa wavuvi eneo la Likoni imejiri siku chache tu baada ya wavuvi kuathirika na shughuli hiyo ya uchimbaji mchanga katika eneo hilo la Likoni.