Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Huku shule zikitarajiwa kufunguliwa siku ya jumatatu, wazazi katika kaunti ya Nakuru wameitaka serikali kupitia wizara ya elimu kuwaepushia mzigo mkubwa wa ununuzi wa vitabu, kama ilivyo ada.

Walisema kuwa wanafunzi wanahitajika kuwa na vitabu vingi vya masoma wanapofungua shule, iwe ni ya msingi au ya upili, ambapo serikali imetakiwa kuingilia kati kuhimiza sekta ya kibinafsi kwa kupunguza bei ya vitabu.

Wazazi waliozungumza na mwandishi huyu mjini Nakuru walisema kwamba wawekezaji wa kibinafsi pamoja na wachapishaji wa vitabu kwenye serikali wanaviuza kwa bei ya juu, ilhali gharama ya maisha inazidi kupanda.

Mzazi Edwin Maina alisema kwamba: “Wazazi hulazimika kukopa pesa kwenye mashirika ya kifedha ama kubadilishana vitabu na wazazi waliokuwa na watoto shuleni” ili kutimiza matakwa yanayotolewa na shule mbali mbali. Walisema mzigo huo huwa mzito kwao haswa baada ya sherehe za krisimasi na mwaka mpya.

Kimani Njoroge kwa upande wake alilalama kwamba katika kila somo wanafunzi wanaitishwa vitabu vingi, ambavyo hukosa maana baada ya kipindi cha miaka miwili au mitatu.