Shirika la maslahi ya watoto la Mission in Action mjini Nakuru limeshtumu wazazi kwa kudorora kwa maadili miongoni mwa watoto.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumamosi, Michael Sasi, kutoka shirika hilo alisema kuwa utafiti wao umebaini kwamba wengi wa watoto hupoteza mwelekeo maishani kutokana na baadhi ya wazazi kutowajibika.

"Ni jambo la kusikitisha sana kwamba baadhi ya wazazi wanakosa kuwalea watoto kwa njia ifaayo na kupelekea watoto wengi kukosa mwelekeo,” alisema Sasi.

Ni kutokana na hilo ambapo afisa huyo wa maswala ya watoto ametaka wazazi kuwajibika vya kutosha katika malezi ya wanao.

Vile vile, ametoa wito kwa serikali kuhakikisha kwamba sheria za mtoto zinalindwa.