Share news tips with us here at Hivisasa

Huku shule zikifunguliwa jumatatu, wazazi katika eneo bunge la Nakuru mjini mashariki wamemrai mbunge David Gikaria kuhakikisha ufadhili wa masomo kupitia basari unawafaidi wanaofaa. 

Mary Njeri, mkazi wa Kivumbini alisema kuwa wakati ni sasa kwa fedha hizo kuwafaidi watoto yatima na wasiyojiweza.

"Mheshimiwa Gikaria anafaa kutushughulikia kwa hii maneno ya basari maanake wakati mwingine fedha hizo hazisaidii wanaofaa," alisema Njeri. 

Naye Henry Bundi, mkazi wa Flamingo anahofia kwamba huenda ufadhili huo ukakosa kuafikia malengo yake iwapo siasa zitaingizwa katika swala hilo. 

"Siasa hazifai kuingizwa katika swala la elimu,"alisema Bundi. 

Matamshi yao yanajiri wakati ambapo Gikaria ametangaza kuwa ufadhili huo na fomu za basari zitaanza kutolewa juma hili katika eneo bunge lake.